Hali ilivyo: Mazishi ya pacha Maria na Consolata Tanzania
Watu wengi wamejitokeza asubuhi ya
leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) eneo la Iringa katika
ibada maalumu ya kuwaaga pacha waliokuwa wameungana Maria na Consolata
waliofariki mwishoni mwa juma.
Miongoni mwa waliofika ni viongozi
mbali mbali wa dini na kiserikali.Baada ya ibada kutakuwa na maandamano
ya kuelekea katika makaburi ya Tosamaganga ambapo ndipo miili yao
itakapopumzishwa.Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amesema vifo vya Pacha hao vinafaa kutumiwa na Watanzania kukumbushana wajibu wao kwa watu wenye ulemavu.
Wameacha somo hilo, tuwajali watu wenye ulemavu hilo ndilo somo walilotuachia Maria na Cobsolata."
Amesema Mungu aliwaumba pacha hao kwa mfano wa sura yake na akawapa uhai kwa kipindi walichokuwa duniani. Vifo vya Maria na Consolata ambao walikuwa ni wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Ruaha vimegusa wengi hasa kutokana na ujasiri walioonyesha wakati wa uhai wao.
Vile vile watakumbukwa kwa ucheshi wao.
Pacha hao wameandaliwa jeneza moja lenye mfumo wa watu wawili, misalaba miwili na watazikwa katika kaburi moja.
Alisema katika uhai wao walichagua kuzikwa kwenye eneo wanalozikwa viongozi wa kanisa Katoliki eneo hilo.
"Wakati wakiumwa walisema wangetamani kuhifadhiwa tunakohifadhiwa sisi hivyo watazikwa kwenye makaburi ya Tosamaganga," alisema.
Kifo chao kiliwagusa wengi Tanzania, wengi wakituma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli, ambaye mapema mwaka huu alikutana na pacha hao, alieleza kusikitishwa kwake na vifo vyao.
"Nimesikitishwa na kifo cha Maria na Consolata. Nilipokwenda hospitali waliliombea taifa. Walikuwa na ndoto ya kulitumikia taifa," aliandika Rais Magufuli kwenye Twitter.
Maisha ya Maria na Consolata
Maria na Consolata Mwakikuti walizaliwa eneo la Ikonda, wilaya ya Makete kusini magharibi mwa Tanzania mwaka 1996.Walisoma shule ya msingi ya Ikonda kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Maria Consolata na baadaye wakasomea hadi kidato cha sita katika shule ya Udzungwa wilaya ya Kilolo.
Septemba mwaka jana, baada ya kufaulu mtihani wa kidato cha sita, walijiunga na chuo kikuu cha kikatoliki cha Ruaha, Iringa.
Walianza kuugua maradhi ya moyo na Desemba wakahamishiwa taasisi ya maradhi ya moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako walilazwa kwa miezi miwili.
Wamekuwa wakitatizwa na afya tangu wakati huo.
"Tulipokea matokeo yetu tukiwa kwenye mazingira ya nyumbani tu, tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, tukaambiwa matokeo yametoka na tumefanya vizuri, tulikuwa tukiwaza kabla ya hapo, unajua kwenye mitihani ya mwisho huwezi kujiamini sana," alieleza Consolata









No comments:
Post a Comment