Trump sasa anatarajiwa kukutana na Kiongozi wa Korea kaskazini kisiwani Sentosa Singapore
Trump sasa anatarajiwa kukutana na Kiongozi wa Korea kaskazini kisiwani Sentosa Singapore
Mkutano unaosubiriwa kwa hamu kati
ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim
Jong-un utafanyika katika hoteli moja kwenye kisiwa cha Sentosa,
Singapore, ikulu ya Marekani imethibitisha.
Mkutano huo wa kihistoria utafanyika Juni 12, lakini taarifa nyingi bado haizjathibitishwa.Itakuwa mkutano wa kwanza kati ya kiongozi wa Korea kaskazini na rais aliyepo madarakani wa Marekani.
Siku ya Jumanne usiku Trump amesema 'mipango inaendelea vizuri'.
"Uhusiano mwingi unaundwa, majadiliano makubwa yanaendelea kabla ya safari," amewaambia waandishi.
Lakini inavyoonekana ni kwamba watakaa katika hoteli tofauti Singapore, kwa mujiu wa ripoti katika gazeti la Straits Times . Hoteli hizo mbili zipo katika kisiwa kikuu .
Sentosa ni mojawapo ya visiwa 63 vya Singapore
Kim Jong-un: Kiongozi mpya mwenye umaarufu katika siasa za Dunia
Ghafla Kim Jong-un amekuwa kiongozi mpya mwenye umaarufu katika siasa za 2018.
Baada ya kuwa kando kwa miaka mingi, ameibuka kuwa kiongozi mwenye nguvu.
Viongozi kutoka China, Urusi, Syria Korea kusini na Marekani wote wamekutana au awanatarajiwa kukutana na Bwana Kim mwaka huu.
"Huu ni mwanzo mpya wa kimataifa ulio tofuati kabisa kuliko tulivyoshuhudia mnamo 2010, wakati Kim Jong Un alipojitokeza kama mtu asiyejulikana, kijana aliyetazamiwa kuwa mrithi wa uongozi.
"Sasa akiwa amejihami kwa silaha nzito, Kim anajitokeza kama kiongozi wa nchi inayojitazama kama nchi yenye nguvu za nyuklia sambamba na nchi nyingine duniani zenye silaha za nyuklia ikiwemo Marekani. " anasema Jean Lee, aliyekuwa mhariri mkuu wa shirika la habari la Associated Press Pyongyang.
Baada ya Kim Jong-un.kutangaza kuwa mapngo wake wa silaha umekamilika, alitangaza kuwa lengo lake kuu ni kushughulikia uchumi.
Na ili kuweza kufanya hivyo alihitaji kuunda uhusiano na kufufua urafiki wa zamani.
Kituo cha kwanza kilikuwa China, mshirika mkuu wa kibiashara wa Korea kaskazini.
Rasi Xi Jinping alisaidia kuidhinisha shinikizo kamili la Donald Trump mwishoni mwa 2017, na kukatiza bidhaa muhimu hatua ambayo iliipa Pyongyang kichefu chefu.
Ilikuwa na hisia zilizoibuka katika mkutano wa kihistoria mnamo Aprili katika mpaka wa Korea na kiongozi wa Korea kusini Moon Jae-in.
Korea Kusini yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini
Ilikuwa ni ziara ya kwanza ya mwanadiplomasi amkuu wa Urusi katika muda unaozidi mwongo mmoja.
Huenda ni sadfa, lakini ni jambo ambalo halikumfurahisha Donald Trump.
Amebadili sheria za mchezo. Mwaka jana alijigamba kwa uwezo wake wa nyuklia, sasa anazitumia kama silaha ya kidiplomasia.
Lakini suali kuu ni je Mchezo huu wa Korea kaskazini utakwishaje? Na ni kitu gani kitakachofanyika baada ya mkutano?
Watu 10 wafariki ajali ya treni na basi Kigoma, Tanzania
Watu 10 wafariki ajali ya treni na basi Kigoma, Tanzania
Watu 10 wamefariki katika ajali
iliyotokea baada ya basi la abiria lililogongana na treni eneo la Gungu
katika manispaa ya Kigoma Ujiji, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu, ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi na mbili na robo asubuhi.Basi hilo la abiria ambalo linamilikiwa na kampuni ya Prince hamida linadaiwa kugongana na treni lilipokuwa linatoka Kigoma Mjini kwenda Tabora.
Treni hiyo ya mizigo ilikuwa ikitoka Kazuramimba kwenda Kigoma Mjini.
Rais wa Tanzania John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kuwtaaka „wadau wote wa usalama barabarani kuchukua hatua madhubuti za kuzuia ajali hizi."
"Vyombo husika, chukueni hatua kali kwa wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani," amesema.
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema eneo ilipotokea ajali hiyo hutokea ajali za aina hiyo mara kwa mara.
"Nimezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC ) na tumekubaliana kuwa tuweke kizuizi ( barrier ) Katika eneo hili ambapo reli ikatiza barabara," amesema.
„ Hii itasaidia sana kupunguza ajali za namna hii. Mkurugenzi wa TRC Bwana Masanja Kadogosa amekubali ushauri huu ambao Wananchi wengi wa Kigoma Mjini wamekuwa wakiutoa."
Hali ilivyo: Mazishi ya pacha Maria na Consolata Tanzania
Hali ilivyo: Mazishi ya pacha Maria na Consolata Tanzania
Watu wengi wamejitokeza asubuhi ya
leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) eneo la Iringa katika
ibada maalumu ya kuwaaga pacha waliokuwa wameungana Maria na Consolata
waliofariki mwishoni mwa juma.
Miongoni mwa waliofika ni viongozi
mbali mbali wa dini na kiserikali.Baada ya ibada kutakuwa na maandamano
ya kuelekea katika makaburi ya Tosamaganga ambapo ndipo miili yao
itakapopumzishwa.Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amesema vifo vya Pacha hao vinafaa kutumiwa na Watanzania kukumbushana wajibu wao kwa watu wenye ulemavu.
Wameacha somo hilo, tuwajali watu wenye ulemavu hilo ndilo somo walilotuachia Maria na Cobsolata."
Amesema Mungu aliwaumba pacha hao kwa mfano wa sura yake na akawapa uhai kwa kipindi walichokuwa duniani. Vifo vya Maria na Consolata ambao walikuwa ni wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Ruaha vimegusa wengi hasa kutokana na ujasiri walioonyesha wakati wa uhai wao.
Vile vile watakumbukwa kwa ucheshi wao.
Pacha hao wameandaliwa jeneza moja lenye mfumo wa watu wawili, misalaba miwili na watazikwa katika kaburi moja.
Alisema katika uhai wao walichagua kuzikwa kwenye eneo wanalozikwa viongozi wa kanisa Katoliki eneo hilo.
"Wakati wakiumwa walisema wangetamani kuhifadhiwa tunakohifadhiwa sisi hivyo watazikwa kwenye makaburi ya Tosamaganga," alisema.
Kifo chao kiliwagusa wengi Tanzania, wengi wakituma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli, ambaye mapema mwaka huu alikutana na pacha hao, alieleza kusikitishwa kwake na vifo vyao.
"Nimesikitishwa na kifo cha Maria na Consolata. Nilipokwenda hospitali waliliombea taifa. Walikuwa na ndoto ya kulitumikia taifa," aliandika Rais Magufuli kwenye Twitter.
Maisha ya Maria na Consolata
Maria na Consolata Mwakikuti walizaliwa eneo la Ikonda, wilaya ya Makete kusini magharibi mwa Tanzania mwaka 1996.Walisoma shule ya msingi ya Ikonda kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Maria Consolata na baadaye wakasomea hadi kidato cha sita katika shule ya Udzungwa wilaya ya Kilolo.
Septemba mwaka jana, baada ya kufaulu mtihani wa kidato cha sita, walijiunga na chuo kikuu cha kikatoliki cha Ruaha, Iringa.
Walianza kuugua maradhi ya moyo na Desemba wakahamishiwa taasisi ya maradhi ya moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako walilazwa kwa miezi miwili.
Wamekuwa wakitatizwa na afya tangu wakati huo.
"Tulipokea matokeo yetu tukiwa kwenye mazingira ya nyumbani tu, tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, tukaambiwa matokeo yametoka na tumefanya vizuri, tulikuwa tukiwaza kabla ya hapo, unajua kwenye mitihani ya mwisho huwezi kujiamini sana," alieleza Consolata














